Featured
- Get link
- X
- Other Apps
JE CINT IMESHAFANYA NINI?
CREATIVE INDUSTRY NETWORK TANZANIA (CINT) ni chombo kilichosajiliwa kihalali, chombo ambacho kinalenga kuwezesha mazingira bora katika tasnia ya Sanaa na Ubunifu, kwa kufuatilia kwa ukaribu mambo ya Sera, Elimu Jinsia, Miundombinu, Uhuru wa kujieleza katika sanaa na mambo mengine yanayohusiana na haya.
Ni nia ya CINT kufanya kazi kwa ukaribu sana na Taasisi mbalimbali, za Kiserikali na za Binafsi, Taasisi za haki za kijamii, wafadhili wa ndani na nje ya nchi, yote hii katika jitihada za kuwezesha wadau na washiriki wa tasnia za Sanaa na Ubunifu Tanzania kupata ufahamu utakaowezesha kazi za Tanzania kuwa na nafasi katika masoko ya duniani. CINT ilianzishwa baada ya vikao kadhaa vya wadau wa sekta ambao waliona pengo la kukosekana kwa chombo kama hiki. Mpaka sasa CINT ndio chombo chenye wanachama wengi katika tasnia ya Ubunifu nchini. CINT ina wanachama katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro, Iringa, Mwanza, Mbeya, Songwe, Dodoma na Arusha. Kuanzia mwaka 2019, CINT imeweza kukutana na mamia ya wasanii na wadau wa sanaa na ubunifu katika mikoa mbalimbali Tanzania, kwa njia hiyo CINT imeweza kupata taarifa nyingi za hali ya sanaa na wasanii katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. Tayari CINT ilikwisha toa jarida la ripoti yake ya kwanza ya mwaka 2019/20, ripoti hiyo iko katika lugha za KIswahili na Kiingereza na karibuni ripoti ya pili itatoka.
![]() |
Jarada la ripoti ya mwaka 2019/20 |
- Get link
- X
- Other Apps
Popular Posts
CINT YATOA TAMKO KUKAMATWA KWA KATIBU WAKE MKUU
- Get link
- X
- Other Apps
LATEST DEVELOPMENTS ON CARTOONIST OPPTERTUS FWEMA CASE.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment